Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chanjo ya TB kwa watoto wachanga wenye VVU inadhuru, kuonya wataalamu Afrika Kusini

Chanjo ya TB kwa watoto wachanga wenye VVU inadhuru, kuonya wataalamu Afrika Kusini

Uchunguzi wa wataalamu wa Afrika Kusini, ambao matokeo yake yalichapishwa kwenye jarida la afya la Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha kwamba ile chanjo kinga dhidi ya kifua kikuu (TB), ambayo kikawaida hupewa asilimia 75 ya watoto wachanga ulimwenguni, baada ya kuzaliwa, inakhofiwa dawa hii huleta madhara kwa watoto walioambukizwa na virusi vya UKIMWI na husababisha hata vifo.

Dawa ambayo  hujulikana kama chanjo ya BCG, imependekezwa wasichanjwe watoto wachanga wagonjwa wa virusi vya UKIMWI kwa sasa hivi. Profesa Simon Schaaf, wa Taasisi ya Desmond Tutu juu ya Tiba ya TB, katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch, Afrika Kusini ambaye ni mshiriki wa utafiti juu ya athari za chanjo ya BCG amenakiliwa akisema "kunahitajika tathmini mpya ya dharura kuhusu natija na madhara ya chanjo ya BCG" kabla haijaendelea kutolewa kuwakinga watoto wachanga dhidi ya ugonjwa wa TB.