Mataifa yanajiandaa kubuni mfumo mpya wa kudhibiti bora mabadiliko ya hali ya hewa

30 Juni 2009

Mkutano wa Tatu wa Dunia juu ya Udhibiti Bora wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa (WCC-3) unatarajiwa kufanyika Geneva, Uswiss kuanzia tarehe 31 Agosti hadi Septemba 04, 2009.

Lengo la kikao hiki ni kuzingatia taratibu za kuanzisha mfumo mpya wa kimataifa, utakaotumiwa kuhudumia athari za mabadiliko ya hali ya hewa na kuzisaidia nchi wanachama kujirekibisha na hali mpya iliojiri hivi sasa kwenye mazingira ya kimataifa. Mfumo huu vile vile utasaidia kuandaa mfumo mpya wa urafiki, utakaokuwa na uwezo wa kuashiria mabadiliko ya hali ya hewa na kuyapatia mataifa fursa ya kujiandaa kudhibiti vyema hatari inayoletwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter