Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hifadhi bora kwa raia walionaswa kwenye mapigano inazingatiwa na Baraza la Usalama

Hifadhi bora kwa raia walionaswa kwenye mapigano inazingatiwa na Baraza la Usalama

Baraza la Usalama limefanyisha kikao cha hadhara Ijumaa kuzingatia ulinzi wa raia kwenye mazingira ya mapigano na vurugu.

Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu, John Holmes alihutubia kikao kwa kudhihirisha takwimu za kusikitisha juu ya maafa ya vifo kwa raia walionaswa kwenye mizozo ya karibuni katika nchi kadha, ikijumlisha Usomali, Afghanistan na JKK. Alisitiza kwamba wenye kuendeleza uhasama dhidi ya raia kwenye maeneo ya mapigano wanawajibika kisheria kufikishwa mahakamani kupewa adhabu wanayostahiki.