Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wawakilishi wa tamaduni za kijadi Afrika Mashariki wazingatia kikao cha mwaka juu ya haki za wenyeji wa asili

Wawakilishi wa tamaduni za kijadi Afrika Mashariki wazingatia kikao cha mwaka juu ya haki za wenyeji wa asili

Wiki hii tutakamilisha makala ya pili ya yale mahojiano yetu na wawakilishi wawili wa jamii za makabila ya wenyeji wa asili kutoka Afrika Mashariki, ambao karibuni walihudhuria kikao cha nane cha ile Tume ya Kudumu ya UM juu ya Haki za Wenyeji wa Asili Duniani kilichofanyika Makao Makuu.

Tume ya Kudumu ya Haki za Wenyeji wa Asili ilikutana kwa muda wa wiki mbili katika mji wa New York, mnamo mwezi Mei, ambapo walkisanyika wawakilishi 2,000 ziada wa makundi ya wenyeji wa asili, kutokea sehemu mbalimbali za ulimwengu, na kujadilia namna ya kuihamasisha jumuiya ya kimataifa kuimarisha haki zao. Miongoni mwa wawakilishi hawo walijumuika wenyeji wa asili wawaili, wenye jadi ya KiMaasai, kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao majina yao ni Adam Kuleti Ole Mwarabu, aliyewakilisha Shirika la Maendeleo ya Wafugaji wa Barakuyo pamoja na Rehema Mkalata, akiwakilisha Shirika la Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake wa Marakuyo. Nilibahatika kufanya mahojiano nao kwenye studio za Redio ya UM. Kwenye makala ya awali, iliopita, wawakilishi hawa wawili walisailia juu ya shughuli za kikao cha mwaka huu, athari za sera za kitaifa kwenye jamii zao, haki za kuendeleza mila katika mazingira ya utamaduni wa kisasa na pia walitathminia haki za wanawake. Makala yaleo tutasikia fafanuzi zao ziada juu ya masuala ambayo wanayapa umuhimu katika utekelezaji wa haki zao kitaifa na kimataifa.

Sikiliza mahojiano kamili kwenye idhaa ya mtandao.