Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

John Holmes ameanza ziara ya siku sita Sudan Kusini na Darfur

John Holmes ameanza ziara ya siku sita Sudan Kusini na Darfur

John Holmes, Naibu KM juu ya Masuala ya Kiutu amewasili Sudan kuanza ziara ya siku sita ili kufanya mapitio juu ya miradi ya kuhudumia misaada ya kihali katika Sudan Kusini na Darfur.

Tangu Serikali ya Sudan kuamua kuwafukuza nchini, mnamo tarehe 04 Machi 2009, wale wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa yasio ya kiserikali 13, ambayo yalihusika na ugawaji wa misaada ya kiutu, UM umeingiwa wasiwasi kuwa umma husika wa maeneo hayo hautoweza kukidhiwa mahitaji yao ya kihali kama inavyotakikana. Holmes anatarajiwa kukutana kwa mashauriano na maofisa wa Serikali ya Sudan, pamoja na timu ya watumishi wakazi wa huduma za kiutu waliopo nchini humo, na pia kukutana na baadhi ya wawakilishi wa kutoka jamii ya wahisani wa kimataifa na mashirika ya kikanda.