Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ILO yasisitiza haja ya kubuniwa ajira wakati wa kufufua uchumi

ILO yasisitiza haja ya kubuniwa ajira wakati wa kufufua uchumi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani ILO amezihimiza serekali za dunia kulenga mipango yao ya kuokoa uchumi katika tatizo la muda mrefu linaloendelea, la ukosefu ajira.

Bw Juan Somavia alitoa mwito huo kabla ya mkutano wa viongozi wa kundi la G20 utakaofanyika London wiki ijayo. Ameeleza uratibu wa kimataifa kukabiliana na mzozo wa kiuchumi duniani umekua ni dhaifu sana, akisema mizizi ya kifedha, biashara, ajira na masuala ya jamii ya mzozo huu wa kimataifa yameingiliana na hivyo ndivyo inabidi sera ipangwe. Akisisitiza juu ya haja ya kuwepo na suluhisho la kimataifa Bw Somavia alisema ukosefu wa kukarabati juhudi za pamoja kutapunguza uwezo jumla wa hatua za kuchochea uchumi na kusababisha kila nchi kutokua tayari kusonga mbele haraka kuliko washirika wake wa biashara na hivyo kuzidisha kuduma kwa uchumi.