Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kukomesha ghasia dhidi ya wanawake asema KM

Lazima kukomesha ghasia dhidi ya wanawake asema KM

KM Ban Ki-moon amerudia tena mwito wake wa dharura wa kukomesha ghasia dhidi ya wanawake akieleza ni adhabu ambayo athari zake ni uchungu usoweza kupimwa.

KM alikua akizungumza wakati UM umeanza mlolongo wa sherehe kuadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake March 8. Alisisitiza kwamba wanawake ndiyo wanao zaa na kuwalea watoto. Katika sehemu kubwa ya dunia wanalima na kupanga vyakula kutulisha. Wana shona nguo tunazo zivaa. Kwa hivyo Bw Ban anasema ghasia dhidi ya wanawake ni shambulio dhidi ya sisi sote. KM aliyeanzisha kampeni mwaka jana ya "Tungane Kukomesha Ghasia dhidi ya Wanawake", alisema moja kati ya kila wanawake watano duniani wanabakwa au kuna jaribio la kubakwa dhidi yao, wakati kuna katikam baadhi ya nchi mwanmke moja kati ya watatu kupigwa au kubughudhiwa. Nae kamishna mkuu wa haki za binada wa UM Navi Paillay amesema vita dhidi ya ubaguzi dhidi ya wanawake, wazawa, watu wa makabila au dini za wachache wahamiaji na makundi mengine ya watu wanaodhuliumiwa vitakua kipau mbele ya idara yake.