Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wahimiza watu kuunga mkono kukomesha biashara haramu ya kuwauza binadamu

UM wahimiza watu kuunga mkono kukomesha biashara haramu ya kuwauza binadamu

UM umezindua kampeni mpya, inayowakilishwa na utepe wa bulu ulochorwa kama moyo katika lengo la kuwahamasisha watu juu ya mamilioni ya waathiriwa wa biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na kuwapatia uungaji mkono kupambana na tabia hii ambayo na utumwa wa mambo leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Kupambana na Madawa ya Kulevya ya UM Antonio Maria Costa alisema kuna hali ya watu kutofahamu utumwa wa kisasa wakati huo huo kuna nia ya kutosha kupambana na tabia hiyo ovu. Utepu wa bulu utawahamasisha watu juu ya uhalifu ambao ni aibu kwetu sote alisema na kuonesha ungaji mkono kwa waathiriwa.