Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za Binadamu na Athari za Mzozo wa Kiuchumi Duniani

Haki za Binadamu na Athari za Mzozo wa Kiuchumi Duniani

Kamishna Mkuu wa haki za binadam Navi Pillay, amezihimiza serekali na wadau wa sekta za kibinafsi kuhakikisha kwamba juhudi zao za kutanzua mzozo wa sasa wa fedha duniani hazita hatarisha haki za binadam. Bi Pillay alisema mzozo wa fedha huwenda ukahujumu uwezo wa kufanya kazi, uwezo wa kumudu chakula na makazi, huduma msingi za afya na elimu. Alisema matokeo ya kuduma kwa uchumi kunaweza kuzidisha chuki dhidi ya wageni na tabia za kibaguzi dhidi ya wafanyakazi wa kigeni huku wasichana na wanawake huwenda wakakabiliwa na ghasia zaidi na ukiukaji wa haki za kiuchumi na kijami.

"Kwa hakika mataifa hayapunguziwi wajibu wao wa haki za binadam wakati wa mizozo. Badala yake, hatua za kulinda siyo tu haki za kiuchumi na kijamii bali pia, ni haki za kiraia na kisiasa za yale makundi na watu watakao athirika zaidi na kutengwa na mzozo huu, zinabidi kuimarishwa kwa dharura na umuhimu."

Kamishna Mkuu alisema hatua za kulinda pamoja na zile za kufufua uchumi na hatua za ukuwaji ni lazima zipangwe kwa kutilia maanani jinsia na zisizo za kibaguzi. Mswada wa azimio ulotayarishwa kabla ya mkutano wa leo unatoa mwito kwa mataifa bila ya kujali athari za mzooz wa kiuchumi duniani kuheshimu wajibu zao za haki za binadam na kulinda haki za kijami.