Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM ahimiza ulimwengu kupigania Haki za Kijamii kwa wote

KM ahimiza ulimwengu kupigania Haki za Kijamii kwa wote

Akiadhimisha kwa mara ya kwanza siku ya haki za kijamii duniani hii leo KM Ban Ki-Moon amesisitiza umuhimu wa kufuatilia haki za kijami kote duniani, akilalamika kwamba watu wengi kabisa hii leo wananyimwa haki hii, ambayo ni moja wapo ya msingi wa UM katika kazi zake za kuendeleza maendeleo na heshima kwa wote.

Amesema kwa usikitifu, haki za kijamii ni ndoto ya mbali kwa idadi kubwa ya binadamu. Akisiistiza kwamba umaskini ulokithiri, njaa, ubaguzi, na kunyimwa haki za binadam ni maqmbo yanayoendelea kuathiri madili zetu. Mzozo wa kifedha duniani amesema unatishia kudhuru zaidi mambo hayo. KM alidokeza kwamba utulivu na ustawi duniani unategemea kuhakikisha watu wanafurahia viwango vinavyokubalika vya maisha bora na usawa kwa wote. Akisema ukosefu wa haki za kijami ni jambo linalobidi kukabiliwa na sisi sote. Siku ya haki za Kijami Duniani tarehe 20 Februari iliidhinishwa na Baraza kuu la UM mwezi Novemba 2007 kutokana na pendekezo la Shirika la Kazi duniani ILO. Hii leo Baraza la Uchumi na Jamii lilijadili juu ya haki za kijamii katika utandawazi wa haki huku katika makao mkuu ya UM mjini New York.