Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu laitisha kikao cha kuzingatia athari za mzozo wa uchumi kimataifa

Baraza la Haki za Binadamu laitisha kikao cha kuzingatia athari za mzozo wa uchumi kimataifa

Raisi wa Baraza la Haki za Binadamu, Martin Ihoeghian UHOMOIBHI, amelezea kwenye mazungumzo na waandishi habari mjini Geneva ya kuwa Baraza litaitisha kikao maalumu Ijumaa ijayo kuzingatia, kwa kina, athari za mzozo wa uchumi kimataifa, hasa katika utekelezaji wa haki za binadamu ulimwenguni.

Alitahadharisha ya kuwa haki za binadamu zinawajibika kushughulikiwa, kwa kikamilifu, nanchi wanachama katika kipindi ambapo walimwengu wanajitahidi pia kukabiliana na matatizo ya kiuchumi katika soko la kimataifa.