Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamisheni ya CSD imeanzisha mijadala ya mwaka Makao Makuu

Kamisheni ya CSD imeanzisha mijadala ya mwaka Makao Makuu

Kuanzia tarehe 05 Mei wanachama wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kudumu (CSD) wamekusanyika kwenye Ukumbi wa Chumba cha 4 cha Mikutano, katika Makao Makuu ya UM, kuendeleza majadiliano ya mwaka katika kikao cha 16, kilichofunguliwa na Naibu KM juu ya Masuala ya Uchumi na Jamii, Sha Zukang. Mada zitakazopewa umuhimu, na kuzingatiwa kwa makini zaidi mkutanoni, ni zile zinazohusika na kilimo, maendeleo ya vijijini, udhibiti wa ukame na kukabiliana na matatizo ya kuenea kwa jangwa pamoja na namna hatua za kuchukuliwa kuisaidia Afrika kupata maendeleo yenye natija kwa umma.