ITU imetoa ripoti mpya kuhusu uekezaji wa mawasiliano ya kisasa Afrika
Ripoti ya Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Mawasiliano ya Kisasa (ITU) iliotolewa mjini Geneva imeelezea viashirio vinavyohitajika siku zijazo kuhusu uekezaji wa mawasiliano bora katika vyombo vya habari barani Afrika. Ripoti ilisailia taarifa za kutumiwa na waratibu wa sera za kitaifa barani Afrika, pamoja na waekezaji wa kimataifa, na vile vile waangalizi na wachanganuzi wa mazingira ya mawasiliano ya Afrika, zitakazowasaidia kuwa na tathmini ya jumla kuhusu sekta za maendeleo.