Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kusaidia wanasiasa Sierra Leone kupata welekevu wa vyombo vya habari

UM kusaidia wanasiasa Sierra Leone kupata welekevu wa vyombo vya habari

Shirika la UM juu ya Miradi ya Maendeleo (UNDP) pamoja na Ofisi ya Kufufua Kadhia za Uchumi na Jamii Sierra Leone (UNIOSIL) yamefanyisha warsha maalumu kwenye mji mkuu wa Freetown, Sierra Leone kuwasaidia wawakilishi wa vyama vya kisiasa kupatiwa uzoefu na welekevu juu ya mbinu za kuwasiliana na umma kwa kueneza ujumbe unaoambatana na itikadi zao za kisiasa, kwa kutumia vyombo vya habari.

Warsha umeongozwa na Kwaku Sakyi-Addo, mwanahabari wa Ghana anayefanya kazi na shirika la habari la Kiingereza la BBC akishirikiana na mwakilishi wa Jumuiya ya Waandishi Habari wa Sierra Leone.