Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yasaidia watoto 60,000 kupata vifaa vya maskuli

UNICEF yasaidia watoto 60,000 kupata vifaa vya maskuli

Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetuma misaada ya vifaa vya skuli kwa wanafunzi watoto 60,000 waliopo kwenye yale maeneo sita ya Zambia yalioathiriwa na mafuriko yaliogharikisha sehemu hizo za nchi hivi karibuni.

Vifaa hivyo vinajumisha misitari, chaki, penseli, kalamu, raba, vitabu vya kuandikia na vifaa vyenginevyo vya skuli ambavyo vitasaidia kuwaliwaza wanafunzi hawa na kupunguza kihoro kiolichowavaa baada ya kushuhudia maafa ya mafuriko nchini mwao.