Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada mpya kwa WFP kuashiria mwisho wa mgawo wa dharura Uganda

Msaada mpya kwa WFP kuashiria mwisho wa mgawo wa dharura Uganda

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imepokea msaada wa yuro milioni 5 kutoka Ofisi ya Misaada ya Kiutu ya Kamisheni ya Ulaya (ECHO) pamoja na mchango ziada mwengineo ambao tuliarifiwa utatumiwa kugawa chakula kwa watu milioni 1.28 waliong\'olewa makwao nchini Uganda. Msaada huu utaipatia WFP fursa ya kurudisha posho kamili ya chakula kwa umma huo muhitaji ambao siku za nyuma walialzimika kupatiwa posho haba kwa sababu ya upungufu wa misaada ya kuendeleza shughuli hizo.

Mchango wa Ofisi ya ECHO ni sawa na dola milioni 6.8, na utatumiwa kununua chakula ndani ya Uganda yenyewe, ili kuwasaidia kiuchumi wakulima wadogo wadogo na pia umma uliokirimiwa msaada huo.