Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lina wasiwasi juu ya mvutano wa Ethiopia/Eritrea

Baraza la Usalama lina wasiwasi juu ya mvutano wa Ethiopia/Eritrea

Baraza la Usalama limeitisha kikao maalumu kusailia ripoti mpya ya KM juu ya hali ya usalama na amani mipakani kati ya Ethiopia na Eritrea. Mkurugenzi wa Kitengo kinachohusika na Masuala ya Afrika katika Idara ya Operesheni za Amani za UM, Dmitri Titov aliiwakilisha ripoti na kuelezea, kwa mukhtasari, matukio yaliojiri karibni kwenye eneo husika la Pembe ya Afrika.

Raisi wa Baraza la Usalama kwa mwezi Mei, Balozi Zalmay Khalilzad wa Marekani aliwaarifu waandishi habari, baada ya mjadala kumalizika, ya kwamba wasiwasi mkuu waliokuwa nao wajumbe wa Baraza hilo unatokana na kupwelewa kwa mpango wa amani kati ya Ethiopia na Eritrea. Walirudia tena kwamba wanaunga mkono kikamilifu kazi na operesheni za Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani katika Mipaka ya Ethiopia-Eritrea (UNMEE) katika kuimarisha hali ya utulivu na usalama wa eneo, na kutoa mwito kwa pande zote mbili husika kushirikiana na operesheni hizo za UM.