Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imeanzisha tena ugawaji wa chakula Mogadishu

WFP imeanzisha tena ugawaji wa chakula Mogadishu

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) imeanzisha tena huduma za kugawa chakula, pamoja na huduma nyenginezo za kihali, kwa wakaazi na wahamaji 16,000 wa Mogadishu, Usomali mnamo wiki hii. WFP ilitarajiwa kuwapatia watu 114,000 msaada wa chakula mnamo mwisho wa wiki, ikijumuisha idadi ya wakazi waliohajiri mji baada ya vita kuanza, pamoja na wale ambao walishindwa kukimbia mapigano na kunaswa ndani ya mastakimu yao wakati uhasama uliposhtadi.