Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yakanusha kushambuliwa kwa raia kambini Malakal

UNMISS yakanusha kushambuliwa kwa raia kambini Malakal

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini umekanusha maoniyaliyotolewa katika safu kunako matoleo mawili ya moja mnamo Juni  30 na Julai mosi  yakituhumu kuwa vikosi vya upinzani juma hili vimekuwa vikishambulia kambiya wakimbizi wa ndani iliyoko katika eneo la ujumbe huo la ulinzi wa raia  jimboni Malakal.

Taarifa ya UNMISS inasema kuwa hakuna ukweli wowote katika madai ya mwandsihi wa safu hiyo kuwa vikosi vya upinzani vinavyomtii makamu wa zamani wa Rais Riek Machar na General wa zamani wa SPLA Johnson Olony, vimekuwa vikishambulia raia katika kambi ya UNMISS ambao wanatoka katika makabila mengine.

Walinzi wa UNMISS wameimarisha ulinzi kuzunguka aneo la kituo cha ulinzi wa raia Malakal kufuatia mashambulizi ambayo yalitokea jimboni Upper Nile juma lililopita umesema ujumbe huo.

Hatua hizo za uimarishwaji wa ulinzi zinakanusha moja kwa moja madai ya mwandishi huyo kuwa raia kituoni Malakal wameachwa chini ya himaya ya vikosi vya upinzani na kwamba hakuna kinachofanywa na  askari walinda amani wa UNMISS