Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yakijita kuimarisha elimu kwa mtoto wa kike Niger

UNICEF yakijita kuimarisha elimu kwa mtoto wa kike Niger

Wakati elimu ikisalia nguzo muhimu ya maendelo ya jamii na nchi kwa ujumla , huko barani Afrika nchini Niger elimu kwa mtoto wa kike imekuwa ni changamoto kubwa kwani wengi wao hawaipati kutokana na sababu mbalimbali.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau kadhaa ikiwemo serikali wanahaha kuwanusuru watoto wa kike kwa kuwapeleka shuleni. Ungana na Flora Nducha katika makala inayoeleza namna UNICEF inavyopambana katika kutekeleza hilo.