Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na kutoafikiwa kwa mkataba wa silaha

Ban asikitishwa na kutoafikiwa kwa mkataba wa silaha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameonyesha kukasirishwa kwake kutokana na wanachama wa Umoja wa Mataifa kushindwa kuafikiana kwenye mkataba ambao utathibiti biashara ya silaha.

Ban amesema kuwa ni jambo la kuhusunishwa kwamba mkutano huo ulichukua majuma manne kukamilika hakuafikiana kuhusu mkataba ambao ungesimamia biashara ya silaha. Mkutano huo ulimalizika siku ya ijumaa uliwaleta pamoja wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa kujadili suala la biashara ya silaha kwenye Umoja wa Mataifa huku ripoti zikisema kuwa baadhi ya nchi zilisema kuwa zinahitaji muda zaidi.