Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban Ki-moon afafanua umuhimu wa vitabu akizindua mkataba Ethiopia

KM Ban Ki-moon afafanua umuhimu wa vitabu akizindua mkataba Ethiopia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezindua mktaba mpya nchini Ethiopia kwa ajili ya kuongeza msukumo wa elimu kwa wanafunzi wa elimu ya msingi huku pia akisherekea mapinduzi makubwa yanayoweza kubadili mitazamo ya vijana kupitia vitabu.

Uzinduzi wa maktaba hiyo umefanikiwa kupitia mbinu za kisasa zilizobuniwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwanufaisha wanafunzi wa elimu ya msingi.

Wakati wa uzinduzi wa maktaba hiyo mjini Addis Ababa Ban alichukua mfano wa maktaba ambayo inajulikana kama “ Ahsante Maktaba Ndogo” na kuikabidhi kwa wahusika wake huku akisema kuwa jamii ya eneo hilo sasa inaweza kufurahia mema.

Maktaba hiyo inatazamiwa kuwanufaisha zaidi ya wanafunzi 1,200 walioko kwenye shule ya msingi ya Keykokeb.

Jumla ya maktaba 110 zimesambazwa katika nchi 15,tangu kuanzishwa kwa mpango wa aina hiyo mwaka 2007 kwa nchi za Afrika