Skip to main content

UM wazindia wiki ya mafungamano ya imani za kidini

UM wazindia wiki ya mafungamano ya imani za kidini

Umoja wa Mataifa umezindua wiki ya kimataifa ya mashirikiano ya imani, kwa

kufanya shunguli mbalimbali ikiwemo kushiriki kupata kifungua kichwa kwa pamoja,

uonyeshaji sinema na kuendesha midahalo ya aina mbalimbali.

Wiki ya mashirikiano ya imani za kidini, kwa mara ya kwanza ilibuniwa na Baraza la Umoja wa Mataifa hapo mwezi Novemba mwaka jana, ilipotangaza kuwa kila wiki ya kwanza ya mwezi wa pili, ni muhimu kuwa na tukio la aina hiyo kwa shabaya ya kuhubiri amani na kuleta utengamao kwa jamii mbalimbali zenye kuamini dini mbalimbali.

Kwenye uzinduzi wa siku hiyo ambayo ujembe wake mkuu ni ule unazingatia maneno yanayohubiri kuwa mpende bwana Mungu wako na jirani yako pia, imewajumuisha pia makundi ya vyama vya kiraia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na vitengo vyake.

Akitoa salama zake kuhusiana na siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa siku hii ni muhimu kwani inatoa fursa kuangazia masuala yanayoikabili dunia na wakati huo huo kudurufu mchango wa viongozi wa dini kuhumiza umoja na utengamano kwenye jamii ambayo inafuata misingi na mifumo ya dini zinazotofautiana.