Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yapinga kunyongwa kwa watu nchini Iraq

Ofisi ya haki za binadamu ya UM yapinga kunyongwa kwa watu nchini Iraq

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa watu 34 wakiwemo wanawake wawili walinyongwa juma lililopita nchini Iraq. Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa kiasi kikubwa cha watu wanaweza kunyongwa kwa siku moja.

Pillay anasema kuwa uhalifu uliotendwa na walionyongwa bado haujulikani. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa zaidi ya watu 1200 wamehukumiwa kifo nchini Iraq tangu mwaka 2004. Rubert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)