Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikusanyiko mikubwa ya watu yatajwa kama hatari kwa afya ya umma

Mikusanyiko mikubwa ya watu yatajwa kama hatari kwa afya ya umma

Shirika la afya dunia WHO limesema kuwa mikusanyiko mikubwa ya watu mara nyingi huwa na athari kwa afya ya umma. WHO imesema kuwa mikusanyiko kama hiyo husababisha hatari kubwa kwa usalama wa afya ikiwa ni hatari ya moja kwa moja kwa umma. Magonjwa yanayosababishwa na joto na kukauka kwa mwili hutokana na kukusanyika kwa idadi kubwa ya watu.

Magonjwa ya kupumua mwa mfano yaliripotiwa kwenye mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi mwaka 2002. Maambukizi ya magonjwa yasiyotarajiwa yanaweza kutokea na hata kusambaa mbali na mikutano mikubwa. WHO imeshirikiana na serikali kadha ili kujiandaa wakati wa mikusanyiko mikubwa kama vile mashindano ya Olimpiki. Dr Maurice Barbechi kutoka kwa kitengo kinachohusika na kutoa onyo la mapema cha WHO anaeleza.

(SAUTI YA DR MAURICE BARBECHI)