Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wakamilisha ziara yake mjini Misrata

UM wakamilisha ziara yake mjini Misrata

Umoja wa Mataifa umekamilisha awamu yake ya pili ya kutathmini hali ya kibinadamu kwenye mji wa Misrata ambao umeshuhudia mapigano makali miezi michache iliyopita wakati wa mzozo nchini Libya. Hata kama mji huo unaonekana kurejea katika hali ya kawaida bado unaendelea kuzungukwa na wanajeshi wa serikali na pia uko kwenye hatari ya kushambuliwa kwa maroketi.

Shughuli hiyo ilitathmini mahitaji ya kibinadamu na usalama kwenye mji huo wa Misrata uliokuwa na takriban watu 517,000 kabla ya mzozo. Ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa uliwajumuisha wafanyikazi kutoka shirika la kuratibu masuala ya kibinadam OCHA , WFP, UNHCR , NICEF na mashirika mengine. Al Khatib ame nena na Radio yaUmoja wa Mataifa kuhusu ziara yake nchini Libya.

(SAUTI YA AL KHATIB)