Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanasiasa tu hawawezi kuleta amani bali pia mchango wa vyombo vya habari: Akasaka

Wanasiasa tu hawawezi kuleta amani bali pia mchango wa vyombo vya habari: Akasaka

Mkuu wa mawasiliano kwenye Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa wale wanaosimamia vyombo vya habari vya kitamaduni na kijamii kutafuta mbinu jinsi wanaweza kuchangia kuwepo kwa mazingira ya amani kwenye eneo la Mashariki ya Kati.

Kiyo Akasaka amesema kuwa ni jambo muhimu kukumbuka kuwa amani sio kitu ambacho kinaweza kuletwa na wanasiasa tu. Akihutubia semina ya kimataifa ya vyombo vya habari kuhusu Mashariki ya Kati mjini Budapest Akasaka amesema kuwa anaamini kuwa makubalino ya kudumu kati ya Israel na Palestina yatapatikana kutokana na jitihada za walioshiriki kwenye Semina hiyo.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)