Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC imeelezea hofu ya matatizo ya wasichana na wanawake Palestina

ECOSOC imeelezea hofu ya matatizo ya wasichana na wanawake Palestina

Baraza la uchumi na jamii ECOSOC limeelezea hofu yake juu ya matatizo yanayowakabili wasichana na wanawake wa Palestina.

Baraza hilo limeridhia waraka unaotoa wito wa kuendelea na nia ya kimataifa ya kuchagiza na kulinda haki za binadamu na pia kuchukua hatua za kuimarisha hali ngumu inayowakabili wanawake na wasichana hao.

Waraka huo umepitishwa kwa njia ya kura ambapo 24 waliunga mkono, watatu ambao ni Australia, Canada na Marekani walipinga na wengine 15 hawakupiga kura kabisa. Baraza hilo limeelezea hofu yake kwa matatizo yanayowakabili wanawake hao hususan wanaoishi maeneo ya Palestina yanayokaliwa ya Mashariki mwa Jerusalem.

Azimio hilo linatoa wito kwa Israel kusaidia kurejea nyumbani kwa wakimbizi wote na wakimbizi wa ndani ambao wengi ni wanawake na watoto wa Kipalestina