Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yameimarisha misaada kwa maelfu ya Wakyrgystan waliosambaratishwa na machafuko

Mashirika ya UM yameimarisha misaada kwa maelfu ya Wakyrgystan waliosambaratishwa na machafuko

Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yamekuwa msitari wa mbele kuwasaidia maelfu ya waathirika wa machafuko nchini Kyrgystan.

Shirika la kutaribu masuala ya kibinadamu OCHA linasema shughuli za misaada bado zinakabiliwa na changamoto kutokana na hali ya usalama, na operesheni za jeshi la serikali zilizoanza mjini Narimani za kuondoa vizuizi. Kwa upande wake shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kuwapa msaada wakimbizi wapatao 100,000 ambao wamevuka mpaka na kuingia nchi jirani ya Uzubekstan. Tani 240 za msaada zikiwemo blanketi, na vifaa vingine zimewasili na kugawiwa kwa wakimbizi.

Nalo shirika la afya duniani linaloratibu msaada wa kimataifa wa afya kwa waathirika walioko Kyrygstan na Uzbekistan, linasema kuwapatia msaada waathirika hao ni changamoto kubwa, ingawa linasisitiza kuwa huduma za afya na hususan kwa waliojeruhiwa ni muhimu sana. Fadela Chaib ni afisa wa WHO

(SAUTI YA FADELA)