Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa kunusuru Yemen juma lijalo-UM

Mkutano wa kunusuru Yemen juma lijalo-UM

Pakua

Kiasi cha dola bilioni 2.1 kinahitajika ili kunusuru maisha ya wakazi wa Yemen, ambako kuna janga kubwa zaidi la kibinadamu kutokana na machafuko, na hivyo Umoja wa Mataifa umeandaa mkutano wa changizo ili kuzipata fedha hizo.

Kwa mujibu wa taarifa kuhusu mkutano huo, Umoja wa Mataifa umeshirikiana na serikali ya Sweden na Uswisi ambapo juma lijalo April 25 mjini Geneva Uswisi, wadau watakusanyika kutoa ahadi hizo, wakati huu ambapo karibu watu milioni 19 wanahitaji usadizi wa kibinadamu na ulinzi.

Wanawake na watoto ndiyo walio hatarini zaidi katika mgogoro huo, imesema taarifa hiyo.

Mgogoro wa Yemen kadhalika ndio unaoongoza kwa dharura ya ukosefu wa chakula duniani, watu zaidi ya milioni 17wakiwa hawana uhakika wa chakula .

Photo Credit
Familia iliofurushwa kufuatia machafuko Yemen wanakula chakula cha mchana huko Al Mazraq, Hajjah, Yemen.(Picha:OCHA)