Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Akina mama na watoto wachanga wakisubiri kuonwa na mkunga katika hospitali ya Ntimaru iliyoko Kehancha, Kaunti ya Migori, Kenya.

Ongezeko la watu duniani ifikapo Novemba 2022 inaweza kuwa baraka au laana

UNFPA/Luis Tato
Akina mama na watoto wachanga wakisubiri kuonwa na mkunga katika hospitali ya Ntimaru iliyoko Kehancha, Kaunti ya Migori, Kenya.

Ongezeko la watu duniani ifikapo Novemba 2022 inaweza kuwa baraka au laana

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Umoja wa Mataifa tarehe 11 mwezi Julai 2022 ilitangaza kwamba idadi ya watu duniani inatarajiwa kufikia bilioni 8 mnamo tarehe 15 Novemba 2022 ikiwa ni hatua muhimu kwa ubinadamu na ikaenda mbali zaidi kutangaza kuwa mwaka 2023 India inakadiriwa kuwa nchi yenye watu wengi zaidi, kuipita China. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani na masuala ya afya ya uzazi UNFPA baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo liliwahoji watu mbalimbali kupata maoni yao kwakuwa wao wanahusika moja kwa moja na idadi ya watu. 

Kwa upande wao suala kubwa zaidi waliloibuka nalo katika ripoti hiyo iliyotolewa na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi na Masuala ya Kijamii UNDESA ni viwango vya uzazi kuwa viko chini kihistoria wakimaanisha “Theluthi mbili ya watu sasa wanaishi katika nchi au eneo lenye viwango vya uwezo wa kufata watoto vya chini ya kiwango cha kupata watoto cha 2.1 kwa kila mwanamke.”

Takwimu hizi mpya zinakuja wakati dunia ikiendelea kupambana na janga linaloendelea la COVID-19 ambalo limeua zaidi ya watu milioni 6 duniani kote, changamoto ya watu milioni 100 waliovunja rekodi kuyakimbia makazi yao kutokana na ghasia, mateso au migogoro,  mabadiliko ya tabianchi yakiwaathiri walio katika hali duni zaidi, na changamoto za wanawake na wasichana kupata haki zao na kwa utu kila mahali. 

Maoni ya Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk. Natalia Kanem kuhusu ongezeko la watu alisema “Watu ndi suluhisho, si tatizo. Nambari ni muhimu, lakini hebu tuhesabu kwa uangalifu. Ulimwengu wenye ustahimilivu wa bilioni 8, ulimwengu unaozingatia haki na chaguzi za mtu binafsi, unatoa uwezekano usio na kikomo - uwezekano wa watu, jamii na sayari yetu ya pamoja kustawi na kustawi.”

Kusoma taarifa ya ripoti ya watu kufikia bilioni 8 bofya hapa 

Mhudumu wa afya akiwatunza watoto wachanga katika idara ya watoto wachanga inayoungwa mkono na UNFPA ya Hospitali ya Al Shaab huko Aden, Yemen.
UNFPA/Ala’a Aldoly
Mhudumu wa afya akiwatunza watoto wachanga katika idara ya watoto wachanga inayoungwa mkono na UNFPA ya Hospitali ya Al Shaab huko Aden, Yemen.

Labda ni neema au laana

Maoni ya taarifa hii yaongezeko la watu pia yalipokelewa kwa muitikio tofauti hususan wa Mashariki ya mbali ambapo kumekuwa kukishuhudiwa kila uchwao vita na changamoto mbalimbali.

Abdulrahman Al-Ward, mwanaharakati wa vijana mwenye umri wa miaka 26 nchini Yemen, amesema mbali na nchi yake kukumbwa na vita visivyokoma amesema. “Pamoja na wazimu unaoendelea ulimwenguni, watu wengi zaidi inamaanisha mateso zaidi.”

Anton Massouh kijana wa miaka 24 mhandishi kutoka Homs nchini Syria yeye ingawa nchi yake ipo kwneye mzozo mbaya zaidi na wamuda mrefu alikuwa na matumaini chanya, “Ulimwengu unaofikia idadi hii utamaanisha sayansi zaidi, uvumbuzi na ugunduzi. Ukuaji huu utachochea teknolojia na utafiti zaidi.”

Kijana mwingine kutoka Yemen ni Musfer ambaye ujumbe wake ulikuwa ni mfupi akisema “Dunia ni ya kila mtu” akimaanisha bila kujali ukubwa wa idadi ya watu duniani, viongozi na watunga sera lazima waendelee kujitolea kwa haki za kila mtu. 

Valentina, mkimbizi wa mwenye umri wa miaka 72 ambaye alikimbia nyumba yake wakati wa vita na Urusi anawasili katika Jamhuri ya Moldova kutafuta usalama. Idadi inayoongezeka ya nchi zinakabiliwa na athari na kutokuwa na uhakika wa idadi ya watu wanaozeeka
© UNFPA Moldova/Eduard Bîzgu
Valentina, mkimbizi wa mwenye umri wa miaka 72 ambaye alikimbia nyumba yake wakati wa vita na Urusi anawasili katika Jamhuri ya Moldova kutafuta usalama. Idadi inayoongezeka ya nchi zinakabiliwa na athari na kutokuwa na uhakika wa idadi ya watu wanaozeeka: Kufikia 2050, watu wenye umri wa miaka 60 na zaidi wanakadiriwa kuwa zaidi ya asilimia 20 ya idadi ya watu ulimwenguni.

Tuwawezesha wanawake na wasichana 

Maoni mengi yaliyotolewa na washiriki kadhaa walitaka kuwawezesha wanawake na wasichana kama mkakati muhimu wa kujenga maisha bora ya baadaye. Mervat Ismail Al-Hijjah, kutoka Homs, Syria, alitoa hoja kwamba katika baadhi ya sehemu za dunia, ndoa za utotoni na mimba za vijana ndizo zinazosababisha viwango vya juu vya uzazi. “Sababu muhimu zaidi ya ongezeko la watu ni ndoa za mapema kwa wasichana wenye umri mdogo, bila kufikiri wala ufahamu,” alisema.

Kauli yake hii inathibitisha utafiti wa hivi karibuni wa UNFPA uligundua kuwa akina mama wanaoanza kuzaa katika ujana mara nyingi wanaendelea kupata watoto wengi zaidi, jambo linaloonyesha kutengwa kwao na ukosefu wa usaidizi. 

Lakini wasichana wanapopata elimu ya kina ya kujamiiana, huduma bora za afya, fursa ya kusoma na kuajiriwa, wanaweza kufanya uamuzi wa upendeleo juu ya kama, lini na nani wapate mimba.

Soma ripoti hiyo hapa 

Uwekezaji mkubwa kama huu wa bwawa katika Mto Nura nchini Kazakhstan mara nyingi unahitaji uwekezaji wa moja kwa moja wa nje.
World Bank/Shynar Jetpissova
Uwekezaji mkubwa kama huu wa bwawa katika Mto Nura nchini Kazakhstan mara nyingi unahitaji uwekezaji wa moja kwa moja wa nje.

Uwekezaji utumie busara zaidi

Wakitazama kuhusu makadirio ya ongezeko la watu na athari zake, suala la uwekezaji liliibuka kutoka kenye mataifa ya Kiarabu, ambapo kuna wasiwasi mkubwa juu ya majanga ya kibinadamu. 

Ibtihal Ait Layachi mkunga katika hospitali ya izazi ya Tetouan nchini Morocco alisema Kukabiliana na majanga ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa maliasili, magonjwa ya milipuko na vita, anaamini kwamba mustakabali wa maisha uko hatarini.

“Nadhani tuko kwenye njia ya kuongezeka kwa idadi ya watu, ambayo inahusishwa na ukosefu mkubwa wa usawa katika mgawanyo wa rasilimali na kasi ya ukuaji wa ulimwengu,” alielezea, ingawa alikiri kuwa changamoto za viwango vya chini vya uzazi vitaleta athari zaidi kwakuwa “Kuna nchi ambapo kuna watu wengi zaidi wamezeeka ni hili ni tatizo kubwa.”

Wengine walikuwa waangalifu zaidi, licha ya magumu ambayo wamepitia na kushuhudia katika maisha yao.

Maimon Musfer, mkufunzi mwenye umri wa miaka 31 katika kituo cha huduma za vijana kinachoungwa mkono na UNFPA huko Taiz, Yemen, alisema idadi hiyo ina ahadi na hatari. “Kufikia watu bilioni 8 ina maana dunia imejaa rasilimali watu, ambao wangeweza kufanya mbingu duniani. Lakini hii inahitaji uwekezaji wa busara wa rasilimali hizo, vinginevyo itakuwa kuzimu bila amani au kuishi pamoja.”

Mfanyakazi mwenzake, Hind Al-Mujahed mwenye umri wa miaka 26, alisema kuwa ubinadamu una uwezo wa sio tu kuishi bali kustawi  ilimradi tu viongozi wajitolee kuhakikisha wanaweka sera zinazofaa. “Tunaweza kuepuka matatizo kama vile ukosefu wa chakula, ukosefu wa ajira, na kadhalika, lakini tu kwa uwekezaji imara katika idadi ya watu, ili waweze kuwa na tija na kukidhi mahitaji ya dunia.”

Kusoma maoni mengi zaidi kwa lugha ya kiingereza bofya hapa