Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Iraq ongezeni juhudi kumaliza mwakamo wa kisiasa:UNAMI

Mitaa ya mji wa Baghdad, Iraq kabla ya kuibuka kwa machafuko
UNAMI
Mitaa ya mji wa Baghdad, Iraq kabla ya kuibuka kwa machafuko

Iraq ongezeni juhudi kumaliza mwakamo wa kisiasa:UNAMI

Amani na Usalama

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq na mkuu wa mpango wa Umoja huo UNAMI amesema kuendelea kupotea kwa Maisha ya vijana na umwagaji damu wa kila siku ni hali ambayo haiwezi kuvumilika nchini humo.

Katika taarifa iliyotolewa leo na UNAMI  mwakilishi huyo maalum Hennis-Plesshaert amesema takriban waandamanaji 467 wameuawa na wengine Zaidi ya 9000 wamejeruhiwa tangu Oktoba Mosi mwaka jana.  Ameongeza kuwa “Ongezeko la vitendo vya matumizi ya riasasi za moto yanayofanywa na vikosi vya ulinzi, ripoti za watu wasiojulikana kuwapiga waandamanaji na kuendelea kwa mauaji ya kupanga ya waandamanaji na watetezi wa haki za binadamu linatisha. Ni muhimu kwa serikali ya Iraq kulinda hali ya uhuru wa kuandamana kwa amani na kuhakikisha kwamba matumizi yoyote ya nguvu yanazingatia viwango vya kimataifa. Pia uwajibikaji ni muhimu, wahusika wote wa mauaji na mashambulizi ni lazima wafikishwe kwenye mkono wa sheria.”

Mwakilishi huyo maalum amesisitiza kwamba mazingira ya hofu na kutoaminiana ytakachokileta ni uharibifu zaidi. Ametaka hatua za kisiasa na mchakato wa kusaka suluhu lazima vichukue nafasi iliyoghubikwa na kutofanya maamuzi ili kuhakikisha ahadi na matakwa ya Wairaq tanatimizwa.

“Kujenga mnepo katika ngazi ya kitaifa na kijamii ndio njia pekee ya kusonga mbele na kuwatoa watu katika mzunguko wa machafuko na kukata tamaa na kiingia katika matumaini”