Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya makusudi ya waandamanaji Iraq ni uhalifu usiokubalika: UNAMI 

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jeanine Hennis-Plasschaert akiwatembelea majeruhi wa maandamano katika hospitali ya al-Kindi mjini Baghdad Iraq (Novemba 2019)
UNAMI/Sarmad al-Safy
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jeanine Hennis-Plasschaert akiwatembelea majeruhi wa maandamano katika hospitali ya al-Kindi mjini Baghdad Iraq (Novemba 2019)

Mauaji ya makusudi ya waandamanaji Iraq ni uhalifu usiokubalika: UNAMI 

Amani na Usalama

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ambaye pia ni mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMI amelaani vikali mauaji ya raia waliokuwa wakiandamana kwa amani mjini Baghdad mapema leo. 

Jeanine Hennis-Plasschaert, amesema mauaji hayo ya kuwapiga risasi raia wasio na hatia yaliyofanywa na makundi yenye silaha yamesababisha vifo na majeruhi wengi miongoni mwa raia .” Mauajihyo ya makusudi kwa waandamanaji wasiokuwa na silaha yyoyote yaliyofanywa na makundiyenye silaha si kingine bali ni unyama wa hali ya juu dhidi ya watu wa Iraq. Wahusika wa ukatili huo ni lazima wabainiwe na kufikishwa mbele ya sharia bila kuchelewa”
Duru za habari zinasema takriban watu 20 wameuawa katika shambulio hilo na wengine wengi kujeruhiwa na tangu kuanza kwa maandamano watu Zaidi ya 400 wameuawa.

Mkuu huyo wa UNAMi ameitaka serikali kufanya kila liwezekanalo kuwalinda watu wanaoandamana kwa amani dhidi ya machafuko yanayofanywa na makundi ya watu wenye silaha yanayoendesha uhalifu wake nje ya mfumo wa serikali.

Pia amewataka wanaoandamana kwa amani kutoa ushirikiano ili kuhakikisha wanalindwa.  Ameongeza kuwa “makundi yanayochangizwa na magene yanayoibuka kutokana na ushwishi wa kutokanje wa kisiasa au yanayotaka kulipiza kisasi yanahatarisha kuiweka Iraq katika hatari kubwa.Ni muhimu kushikamana ili kulinda haki za msingi kama haki ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kuongea.”
Mwakilishi huyo maalum pia ametuma salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kuwatakia ahuweni ya haraka waliojeruhiwa katika shambulio hilo.