Kudai haki zao kunawalipisha gharama kubwa raia wa Iraq: Hennis-Plasschaert

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jeanine Hennis-Plasschaert akiwatembelea majeruhi wa maandamano katika hospitali ya al-Kindi mjini Baghdad Iraq (Novemba 2019)
UNAMI/Sarmad al-Safy
Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Jeanine Hennis-Plasschaert akiwatembelea majeruhi wa maandamano katika hospitali ya al-Kindi mjini Baghdad Iraq (Novemba 2019)

Kudai haki zao kunawalipisha gharama kubwa raia wa Iraq: Hennis-Plasschaert

Amani na Usalama

Raia wa Iraq wanaendelea kubeba gharama kubwa ya kutaka sauti zao na madai yao yasikike amesema mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa Iraq UNAMI.

Jeanine Hennis-Plasschaert akuzungumza kwenye Baraza la Usalama hii leo kuhusu hali nchini Iraq amesema tangu mapema mwezi Oktoba mwaka huu Zaidi ya watu 400 wameuawa na wengine zaidi ya 19,000 wamejeruhiwa katika machafuko yaliyochangiwa na maandamano makubwa.

Amesema maanadamano hayo awali yalianzishwa na vijana waliotaka kupaza sauti zao kutokana na hali mbaya ya uchumi, kijamii na matarajio ya kisiasa wakitoa sauti ya matumaini ya kuwa na mustakbali bora hapo baadaye ambao uko mbali na ufisadi, kuingiliwa na siasa za nje na matakwa ya wachache.

Ameongeza kuwa maelfu ya raia wa Iraq kutoka katika kila hali ya maisha walimiminika mitaani  kwa mapenzi ya taifa lao wakihimiza hadhi ya Uiraq wao na wanachokiomba ni taifa hilo kufikia uwezo wake kwa faida ya Wairaq wote.

Ndani ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jeanine Hennis-Plasschaert (kwenye video ukutani), akilieleza Baraza kuhusu hali ya Iraq
UN Photo/Eskinder Debebe)
Ndani ya ukumbi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Jeanine Hennis-Plasschaert (kwenye video ukutani), akilieleza Baraza kuhusu hali ya Iraq

 

Matakwa ya Wairaq

Mkuu huyo wa UNAMI amnesema cha kusikitisha ni kwamba hali bado ni mbaya na “Tunapowakumbuka waliopoteza maisha na kuwaenzi mawazo yao na madai yao bado yako hai sasa kuliko wakati mwingine wowote. Mmoja wa waandamanaji aliniambia bayana kwamba am ani maisha ya utu na uhuru au kutokluwa na Maisha kabisa , na hii ndio sababu ya maandamano.”

Amesema amepata fursa ya kuzungumza na wazazi mbalimbali waliojawa na hofu kuhusu maisha na mustakbali wa vijana wao mmoja wa mama wa kijana wa miaka 16 aliyejeruhiwa vibaya kwenye maandamabno akiwa kitandani kwa mwanaye alimwambia mkuu wa UNAMI kwamba “Kutokuwepo na matarajio ndiko kunakowafanya vijana wetu kuwa na hamasa, kunawafanya kufikiri na kuchukua hatua ambazo zinazidi umri wao mara mbili.”

Ameongeza kuwa kijana wake ana miaka 16 tu lakini ni miaka mingi kwa mtu anayesubiri kwa viongozi wa siasa kutimiza ahadi yao.

Kwa mujibu wa Hennis-Plasschaerthivi sasa "vijana hawa hawakumbuki Maisha yaliyokubwa mabaya wakati wa Saddam Hussein . Hata hivyo wanafahamu fika maisha ambayo waliahidiwa baada ya saddam Hussein . Na kwa kupitia nguvu ya mawasiliano wanajua fika kwamba mustakbali bora unawezekana. Mara nyingi mie husema hali ya sasa inaweza kuzungumziwa bila kutumbukiza yaliyopita Iraq, lakini tunachokishuhudia ni mkusanyiko wa kupagawa kutokana na ukosefu wa maendeleo kwa miaka mingi.”

Amesisitiza kwamba taifa lolote lenye mafanikio linahitaji kukumbatia uwezo wa vijana wake na kwa Iraq hili ni la msingi sana kwa watu wake ambao asilimia kubwa ni vijana.

Jeanine Hennis-Plasschaert mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya Iraq na mkuu wa UNAMI akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama kuhusu hali ya Iraq.
UN Photo/Cia Pak
Jeanine Hennis-Plasschaert mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kwa ajili ya Iraq na mkuu wa UNAMI akitoa taarifa kwenye Baraza la Usalama kuhusu hali ya Iraq.

Mambo yalivyo Iraq

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amesema hali imezidi kuwa mbaya hivi karibuni na serikali ikaamua kuchukua suluhu ya kutumia nguvu na hivyo kuchangia kupotea kwa maisha ya watu wengi, majeruhi, na ghasia na ukichanganya na ahadi hewa za miaka mingi basi yote hayo yamefanya kuwa na mgogoro mkubwa wa kutokuwa na imani.

Ameongeza kuwa “ingawa serikali imetangaza mabadiliko kadhaa kushughulikia matatizo kama ya nyumba, ajira, msaada wa kifedha na elimu , mara nyingi haya huchukuliwa kama si kweli au yamechelewa. Lakini pia uchunguzi wa serikali kuhusu machafuko ya Oktoba unaonekana haujakamilika. Nani anasambaratisha vyombo vya Habari? nani anawapiga risasi waandamanaji?, kuwateka raia? Hawa watu wenye vinyago usoni na silaha ni kina nani? Walenga shabaha wasiojulikana? Watu wenye silaha wasiojulikana?”

Pia mwakilishi huyo amesema anajua kwamba kuna idadi ya vibali kadhaa vya watu kukamatwa vilivyotolewa lakini anapenda kusisitiza kwamba wahusika ni lazima wawajibishwqe kikamilifu.

Ukweli ulio bayana

Mwakilishi huyo amesema ingawa hakutoweza kuwa na sababu yoyote ya kuhalalisha mauaji na majeruhi kwa wanaoanfdamana kwa amani , haya ndio mambo ambayo UNAMI imekuwa ikiyaorodhesha na wakati sheria ni kuhakikisha kunapunguzwa matumizi ya nguvu kupita kiasi “ukweli mchungu ni kwamba risasi za moto, mabomu ya kutoa machozi na ukamatwaji wa watu kiholela na kuswekwa rumande vinaendelea sambamba na utekaji, vitisho na kudhalilisha watu.”

Hivyo Bi Hennis-Plasschaert amerejelea kusisitiza umuhimu wa kuhakikishwa haki za msingi kuanzia haki ya kuishi, lakini pia ya kukusanyika kwa amani na uhuru wa kujieleza.

Ametaja kuwa kufungiwa kwa vyombo vya Habari, intaneti na mitandao ya kijamii kumeongeza mtazamo kwa jamii kwamba malaka ya nchi hiyo ina kitu cha kuficha. Amesisitiza kwamba kukabiliana na hotuba za chuki hakumaanishi kuzuia au kukataza uhuru wa kujieleza.

Amesema waandamanaji wanatsaka mustakabali bora “Na ni jukumu la serikali kuwalinda watu wake na kwamba mifumo yote ya ghasia na machafuko haivkubaliki wala kuvumilika na haipaswi kuingilia haki ya msingi ya kudai mabadiliko. Na ukweli ni kwamba waandamanaji wamedhamiria kuendelea hadi pale madai yao yatakapotimizwa.”

Ameonya kwamba hali hiyo haiwezi kutatuliwa kwa kuvuta muda au suluhu za juujuu na matumizi ya nguvu kwani mtazamo huu utachochea Zaidi hasira za wat una kutokuwa na imani na mamlaka.