Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili kwa mpango wa kibinadamu nchini Syria wapokea asilimia 50- OCHA

Syria
OCHA Syria
Syria

Ufadhili kwa mpango wa kibinadamu nchini Syria wapokea asilimia 50- OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Mpango jumla wa hatua za kibinadamu nchini Syria unahitaji karibu dola bilioni 3.3 na kwa sasa umefadhiliwa kwa asilimia 52 kwa jumla, kwa mujibu wa msemaji wa OCHA Jens Laerke.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Laerke alisema kuwa  Zaidi ya dola bilioni 1.7 zimepokelewa ambapo wafadhili wakuu wakiwa ni Marekani dola milioni 688, Ujerumani dola milioni 262, Uingereza dola milioni 148, Tume ya Ulaya dola milioni 99 na Canada dola milioni 80 kwa mujibu wa OCHA.

Kwa jumla ufadhili unaohitajika dhidi ya hali iliyo nchini Syria kwa mpango mzima wa kibinadamu  kwa sasa unafiakia dola bilioni 4.7.

Kwa miradi kadha iliyo katika mpango huo, baadhi imepata pesa kidogo:

Ombi kwa ajili ya makazi na bidhaa zisizo za chakula limepokea asilimia 9.4 ya milioni 527 zilizoombwa; usalama umepokea asilimia 11.4 ya dola milioni 353 zilizoombwa; maji na usafi imepokea asilimia 12.1 ya dola milioni 274 zilizoombwa; Afya imepokea asilimia 21.2 ya dola milioni 449 zilizoombwa na Elimu imepokea asilimia 26.5 ya dola milioni 252 zilizoombwa.

Sekta iliyoombewa kiwango kikubwa zaidi ya fedha ni chakula ikihitaji dola bilioni 1.1 na hii tayari imechangiwa kwa kiasi kikubwa kwa kupatiwa dola  milioni 574 au asiliamia 53 ya ombi.

Na maeneo mengine ambayo ombi lililoombwa na kiwango kilichopatikana ni zaidi ya asilimia 50 ni lishe, mawasiliano  ya dharura na operesheni na usimamizi.