Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 202 zahitajika kwa ajili ya msaada wa kibinadamu Libya 2019:OCHA

Mohammed mwenye umri wa miaka 16 anaishi Al Saberi huko Benghazi, yeye na jamaa zake walikimbia nyumbani kwao wakati makazi yao yalishambuliwa wakati wa vita 2015.
UN OCHA/GILES CLARKE
Mohammed mwenye umri wa miaka 16 anaishi Al Saberi huko Benghazi, yeye na jamaa zake walikimbia nyumbani kwao wakati makazi yao yalishambuliwa wakati wa vita 2015.

Dola milioni 202 zahitajika kwa ajili ya msaada wa kibinadamu Libya 2019:OCHA

Msaada wa Kibinadamu

Umoja wa Mataifa pamoja na serikali Libya leo wamezindua ombi kwa ajili ya mipango ya kutoa huduma za kibinadamu kwa mwaka 2019. Ombi hilo ni la dola milioni 202 zitakazotumika kutoa msaada wa huduma za afya, ulinzi,maji na masuala ya usafi, malazi na elimu kwa watu zaidi ya 550,000 wasiojiweza.

Akizungumzia ombi hilo mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva uswis hii leo msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA bwana Jens Laerke, amesema miaka saba ya machafuko yimeleta athari kubwa kwa maelfu ya Watoto, wanawake na wanaume nchini Libya na leo hii maelfu ya familia haziwezi kumudu chakula, maji wala vifaa vingine vya msingi nyumbani. Na kuonmgeza kuwa

(SAUTI YA JENS LAERKE)

“Takriban watu 823,000 kote Libya ikiwa ni pamoja na Watoto robo milioni wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hii inajumuisha wakimbizi wa ndani na watu wanaorejea, watu walioathirika na vita, jamii zinazowahifadhi , wakimbizi na wahamiaji ambao wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili kutokana na kutokuwepo utawala wa sharia.”

 Ameongeza kuwa asilimia kubwa ya watu wanaohitaji msaada wanaishi katika maeneo ya mijini yaliyofurika watu hususan mikoa ya Mashariki na Magharibi mwaLibya. Hata hiyo ameeleza kuwa watu wanaohitaji msaada zaidi ni wale walioko katika maeneo ya pwani ya Sirt nan a maeneo ya Kusini mwa nchi ya Murzuq, Sebha na  Alkufraambako fursa ya kufika ni finyu kutokana na  ukosefu wa usalama.

Fedha zinazoombwa mwaka huu kwa mujibu wa OCHA zitasaidia kuhtoa huduma za ulinzi kama vile elimu kwa Watoto na jamii kuhusu hatari ya mabomu yalyotegwa ardhini na msaada maalumu kwa waathirika wa vilipuzi. Pia fedha zikipatikana na kutosha OCHA inasema kutaundwa timu ya dharura ya matibabu na kupeleka madaktari katika maeneo ambako wahudumu wa afya ni hafifu. Vituo vya maji safi na usafi pia ni masuala yanayopewa kipaumbele cha juu.