Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya watu milioni 20 hatarini kwa tisho la baa la njaa Yemen-UN

Katika kituo cha afya cha uzazi Al Sabeen Sana'a Yemen, WFP inatoa lishe iliorutubishwa kutibu mtoto Ali Yakya Ali anayeugua utapiamolo uliokithiti wakati babake akifuatilia. Novemba 2018
WFP/Marco Frattini
Katika kituo cha afya cha uzazi Al Sabeen Sana'a Yemen, WFP inatoa lishe iliorutubishwa kutibu mtoto Ali Yakya Ali anayeugua utapiamolo uliokithiti wakati babake akifuatilia. Novemba 2018

Maisha ya watu milioni 20 hatarini kwa tisho la baa la njaa Yemen-UN

Msaada wa Kibinadamu

Hali mbaya ya uhakika wa chakula inayoongezeka haraka nchini Yemen inaweka rehani Maisha ya karibu watu milioni 20 kwa mujibu wa tathimini ya uhakika wa chakula (IPC) iliyotolewa leo na serikali ya Yemen, Umoja wa Mataifa washirika wa misaada ya kibinadamu.Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema msaada wake wa chakula ndio msaada pekee unaoepusha janga kubwa la baa la njaa nchini humo lakini mapigano yanayoendelea, kupanda kwa beiza vyakula na kuporomoka kwa uchumi viwanawasukuma watu kuelekea kwenye baa la njaa.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa WFP David Beasley tathimini hiyo ni ya kusikitisha “inadhihirisha hofu yetu kwamba watu wanakufa kwa njaa Yemen, idadi ya watu walio katika hatihati ya kukumbwa na baa la njaa imeongezeka mara mbili, tunahitaji msaada na tunauhitaji sasa, la sivyo familia zisizo na hatia, watoto wa kike na wa kiume watakufa.”

Matokeo ya tathimini hiyo ya IPC yanaonyesha kwamba kinachotokea Yemen ni mgogoro uliokita mizizikukiwa na watu milioni 15 walio katika hali mbaya ya njaa na miongoni mwao 65,000 wanakabiliwa na hali ya njaa ambayo inaelezewa kuwa baa.

WFP inasema imekuwa ikiwafikia zaidi ya watu milioni 7 wakio katika hali mbaya ya njaa kila mwezi ikiwapatia msaada wa chakula na linaongeza jitihada kuwafikia takriban watu milioni 12 wanaohitaji msaada wa dharura wa chakula na lishe.

Lakini limeongeza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni fursa , imefanikiwa kuepusha baa la njaa katika baadhi ya sehemu  ilizoweza kufika , na maeneo ambako watu wanakabiliwa na baa la njaa ni katika maeneo ya mapigano ambako hawana fursa ya kufika mara nyingi.

Hivi sasa WFP inasema juhudi kubwa zilizopangwa kufanyika kuepusha baa la njaa zinahitaji ufadhili wa fedha , kwas asa wana akiba ya kutosha ya chakula nchini humo lakini wanahitaji dola milioni 152 kwa mwezi ili kuweza kuendelea na kampeni hiyo kwa mwaka ujao.

 

TAGS:WFP, njaa, Yemen, msaada , chakula, IPC