Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwarejesha watoto kinguvu huko Amerika ya Kusini kwazidisha umaskini na ghasia- Unicef

Vijana matineja waliorejeshwa ka nguvu kutoka Mexico wawasili katika kituo cha serikali cha kuwahifadhi.
UNICEF/Tanya Bindra
Vijana matineja waliorejeshwa ka nguvu kutoka Mexico wawasili katika kituo cha serikali cha kuwahifadhi.

Kuwarejesha watoto kinguvu huko Amerika ya Kusini kwazidisha umaskini na ghasia- Unicef

Wahamiaji na Wakimbizi

Ghasia za kupindukia, umaskini na ukosefu wa fursa siyo huchochea uhamaji holela wa watoto kutoka maeneo ya kaskazini mwa Amerika ya Kusini na Mexico, bali pia ni matokeo ya watoto kufurushwa kutoka Mexico na Marekani, imesema ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa. 

Nchini Guatemala pilikapilika katika moja ya vituo vya kupokea wahamiaji

Pilar,Umri 15 na familia yake wakiwa ndani ya chumba wanachokodi mjini Guatemala. Pilar na familia yake walikimbilia Honduras baada ya genge  kuwatishia  ikiwa Pilar hatakubali kuwa kahaba wa gaenge hilo.

Idadi kubwa hapa ni vijana na msichana mmoja amemkumbatia kaka yake mkubwa ambaye amerejeshwa nyumbani.

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Guatemala, Honduras na Mexico ni nchi ambazo kwazo watoto wanalazimika kukimbia ili kuokoa maisha yao. Mary mmoja wa waliorejeshwa anasema..

Hapa kuna ghasia nyingi. Mtu mmoja anafariki dunia kila baada ya siku tatu au nne.Ni hatari sana kutoka nje usiku saa tatu.”

Kijana mwingine kwa jina la Zoe ambaye baba yake alimsaidia kuondoka, akafunguka.

 “Baba yangu alifanya hivi ili kutulinda kwa sababu anapenda maisha yetu yetu yawe bora. Kila baba anatamani hivyo kwa watoto wake. Kwa hiyo nilimwambia nataka kuondoka hapa kwa sababu tunaishi kwenye nchi hatari. Awali ilikuwa tulivu lakini si hivyo tena. Kila unachosikia kila wakati ni mauaji ya vijana kama mimi.”

Akinukuliwa kwenye ripoti hiyo iliyopatiwa jina waliofurushwa Amerika ya Kati na Mexico Mwakilishi wa UNICEF kanda ya Amerika ya Kusini na Karibea Maria Cristina Perceval, amesema vijana wengi wanaorejeshwa nyumbani kutoka Mexico na Marekani hukabiliwa na  unyanyapaa kwa kuwa mipango yao ya kuhamia nje ya nchi haikufaulu.

Halikadhalika ghasia na pia umaskini kwa kuwa huwa wanachukua mikopo kufanikisha safari za nje na kwa kuwa wanarejeshwa hujikuta hawana pa kufikia wala pesa za kujikimu.

Mama akitokwa machozi akisubiri kukutana na mtoto wake wa kiume ambae amerejeshwa kwa nguvu kutoka Mexico.
UNICEF/Tanya Bindra
Mama akitokwa machozi akisubiri kukutana na mtoto wake wa kiume ambae amerejeshwa kwa nguvu kutoka Mexico.

Bi. Perceval amesema ni muhimu kushughulikia hatari zinazopata vijana na watoto hao wanaorejea na kwamba serikali zichukue hatua sahihi.

Mathalani mikakati ya kutatua sababu za kukimbia, kuwapatia watoto huduma muhimu wakati wa harakati za uhamiaji, kuwasaidia na mipango ya kujumuika tena na jamii zao pamoja na kuhakikisha kurejeshwa nyumbani kwa mtoto kunafanyika kwa maslahi yake na si vinginevyo.