Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zisiweke rehani haki za wahamiaji kwa madai ya hofu ya usalama:UN

Wakimbizi kutoka Amerika ya Kati akiwa Mexico.
© UNHCR/Markel Redondo
Wakimbizi kutoka Amerika ya Kati akiwa Mexico.

Nchi zisiweke rehani haki za wahamiaji kwa madai ya hofu ya usalama:UN

Wahamiaji na Wakimbizi

Wakati msafara wa mamia ya raia wa Amerika ya Kati ukiripotiwa kuvuka mpaka na kuingia Mexico mwishoni mwa wiki, mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, Felipe Gonzalez, ametoa wito kwa nchi kutoziweka rehani haki za binadamu za wahamiaji hao kwa  sababu ya hofu ya masuala ya usalama.

Katika mahojiano maalumu na UN News, bwana Gonzales amesema msafara huo kutoka Amerika ya Kati ni mfano mmoja tu wa hali inayotokea kila siku katika maeneo mengi duniani na kuzusha mjadala unaoendelea wa mkataba wa kwanza wa kimataifa kuhusu wahamiaji unaotarajiwa mwezi Desemba utakavyosaidia changamoto hii . Kufuatia wimbi hilo la wahamiaji wa Amerika ya Kati amessiitiza kwamba

(SAUTI YA FELIPE GONZALEZ CUT 1)

  “Ni muhimu kufikiria kwamba sio kwa bahati mbaya msafara wa watu wote hawa wanakuja nchini Marekani, hii ni kutokana na hali mbaya wanayokabiliana nayo katika nchi wanakotoka, hivyo natoa wito kwa nchi kutochukua hatua kutokana na hofu ya usalama bali kutilia maanani haki za binadamu.”

Na je mkataba wa kimataifa wa uhamiaji unaosubiriwa kwa hamu mnamo Desemba utaleta ahuweni yoyote katika zahma hii?

(SAUTI YA FELIPE GONZALEZ CUT 2)

“Hicho sio chombo cha haki za binadamu lakini ni sehemu ya haki za binadamu , hivyo nadhani ni hatua muhimu, na nadhani utendaji wa mkataba huo wa kimataifa wa uhamiaji utategemea na aina ya utekelezaji itakayofanyika na utayari wa nchi na Umoja wa Mataifa kusonga mbele katika suala hili.”

 

TAGS: Amerika ya Kati, Wahamiaji, Felipe Gonzalez, Marekani, Mexico.