Tanzania kuendelea kuwa 'muumini' wa ushirikiano wa kimataifa- Rais Samia
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amehutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani ikiwa ni mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo mwezi Machi mwaka huu, huku akimulika masuala mbalimbali kuanzia uchumi, siasa, tabianchi, COVID-19 na usawa wa jinsia.