26 Septemba 2017

Kituo cha biashara cha kimataifa kilicho chini ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kiliandaa mikutano kadhaa kando mwa mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, #UNGA72 uliofikia tamati siku ya Jumatatu.

Katika moja ya vikao hivyo, washiriki walipata maelezo ya mafanikio ya mpango wa UNCTAD wa #SheTrades ambao unatoa jukwaa kwa wanawake wajasiriamali kubadilishana taarifa na bidhaa wanazouza kupitia intaneti. Miongoni mwa walioshiriki vikao hivyo ni Dkt. Josephine Ojiambo, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola ambaye katika makala hii anaanza kwa kumweleza Assumpta Massoi kile ambacho kiliwakutanisha.

 

Mahojiano ya Assumpta Massoi kuhusu Jumuiya ya Madola kusongesha maendeleo ya wanawake, by UN News Kiswahili

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud