Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kilimanjaro mila na desturi bado ni kikwazo cha haki ya mwanamke:Minde

Elizabeth Maro Minde kutoka katika shirika la kijamii linalojikita na haki za binadamu na jinsia liitwalo Kilimanjaro Women Information and Community Organization katika mahojiano kandoni mwa CSW63.
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya
Elizabeth Maro Minde kutoka katika shirika la kijamii linalojikita na haki za binadamu na jinsia liitwalo Kilimanjaro Women Information and Community Organization katika mahojiano kandoni mwa CSW63.

Kilimanjaro mila na desturi bado ni kikwazo cha haki ya mwanamke:Minde

Wanawake

Mila na desturi zimeendelea kuwa mtihani mkumu katika juhudi za ukombozi wa mwanamke katika kupata haki na sheria  sehemu mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania, kwa nini? 

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa suala hilo ni mtambuka na ndio maana nchi wanachama zinahimizwa kuhakikisha zinatokomeza mila na desturi hizo kabla ya mwaka 2030 ili kutimiza ajenda ya maendeleo endelevu inayosisitiza kutomuacha yeyote nyuma husuan mwanamke. Nchini Tanzania jitihada kubwa zinazofanyika lakini katika baadhi ya maeneo ikiwemo mkoa wa Kilimanjaro mila na desturi zimeendelea kuwa kikwazo na si suala geni kwa mujibu wa Elizabeth Maro Minde kutoka katika shirika la kijamii linalojikita na haki za binadamu na jinsia liitwalo Kilimanjaro Women Information and Community Organization.  Kazi yake kubwa ni kuhamasisha na kuelimisha jamii hususani wanakwake kuhusu haki zao kisheria na jinsi ya kuzidai . Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano kamisheni ya hali ya wanawake duniani amenifafanulia kuhusu sheria hizo za kimila

(MAHOJIANO NA ELIZABETH MARO MINDE)