Elimu ni mkombozi kwa msichana wa kimasai- Mamasita

Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW62 umeanza makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kubwa zaidi linaloangaziwa ni wanawake na wasichana wa vijiji. Wawakilishi wa mashirika ya kiraia wamefika na miongoni mwao ni Maria Mamasita kutoka Monduli mkoa wa Arusha nchini Tanzania.
Ukosefu wa usawa kati ya maeneo ya mijini na vijijini ni kikwazo kwa maendeleo ya jamii. Na tofauti hiyo inazidi zaidi pindi jamii hiyo ina wanawake ambao kwao mahitaji yao yanapuuzwa licha ya kwamba wana mchango mkubwa katika maendeleo ya jamii zao. Kutoka Arusha Tanzania, Assumpta Massoi amezungumza na Maria Mamasita mshiriki wa mkutano wa 62 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW62 ulioanza tarehe 12 mwezi huu wa Machi, mada kuu ikiangazia kumwendeleza mwanamke wa kijijini. Je wao wanafanya nini?