Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

13 OKTOBA 2020

Katika jarida la habari la Umoja wa Mataifa  hii leo, Flora Nducha anakuletea

-Katika siku ya kimataifa ya kupunguzahatari za majanga Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres  ameonya kwamba bila udhibiti mzuri wa hatari za majanga , hali ambayo ni mbaya itazidi kubwa mbaya zaidi

-Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, IFAD, WHO na ILO leo katika taarifa yao ya pamoja yameonya kwamba COVID-19 mbali ya kuathiri afya inaathiri maisha ya watu na mifumo ya chakula hivyo hatua zichukuliwe haraka kunusuru janga zaidi

Sauti
11'42"