13 OKTOBA 2020
Katika jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo, Flora Nducha anakuletea
-Katika siku ya kimataifa ya kupunguzahatari za majanga Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres ameonya kwamba bila udhibiti mzuri wa hatari za majanga , hali ambayo ni mbaya itazidi kubwa mbaya zaidi
-Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya FAO, IFAD, WHO na ILO leo katika taarifa yao ya pamoja yameonya kwamba COVID-19 mbali ya kuathiri afya inaathiri maisha ya watu na mifumo ya chakula hivyo hatua zichukuliwe haraka kunusuru janga zaidi
-Shujaa wa elimu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, mwalimu kutoka Uturuki anasema pamoja na kukatishwa tamaa na janga la COVID-19 wanafunzi wake ambao ni watoto wakimbizi kutoka Syria walimpa nguvu ya kuendfelea kufundisha
-Makala yetu leo inatupeleka Kilimanjaro Tanzania kwa mama mkulima wa pilipili kupitia msaada wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP
-Na mashinani tunakwenda Kenya kwa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA, ambapo utamsikia binti akieleza changamoto za mbimba za utotoni