Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Masoko ya hisa duniani yamekuwa yakishuka thamani kadri mlipuko wa virusi vya corona unavyozidi.
UN Photo/Mark Garten)

Ukuaji wa uchumi duniani watishiwa na COVID-19:UNCTAD

Mgogoro wa kimataifa wa kiafya uliosababishwa na janga la virusi vya corona au COVID-19 unaweza kuwa na athari kubwa za kiuchumi, na kusababisha upungufu wa dola bilioni 2, 000, pamoja na dola bilioni 200 kwa nchi zinazoendelea, kulingana na moja ya matarajio mabaya yaliyotolewa leo Jumatatu kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD huko Geneva Uswis.

09 MACHI 2020

CSW64 ni fursa ya kuchagiza kasi ya kufikia usawa wa kijinsia, umesema Umoja wa Mataifa. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, baadhi ya wanawake waliopona ugonjwa wa Ebola wametoa shukrani zao kwa mamlaka. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema idadi ya watoto waliovuka pori la Darien linalotenganisha Colombia na Amerika ya Kati mwaka 2019 imeongezeka zaidi ya mara saba. 

Sauti
12'30"