michezo

Michezo ina mchango muhimu katika amani na maendeleo ya Burundi 

Wananchi wa Burundi wameshukuru wazo la Umoja wa Mataifa kuchagiza michezo wakidai imekuwa na mchango katika kurejesha amani nchini mwao kwa kuziunganisha pande zilizokuwa zinakinzana katika masuala ya kisiasa na kijamii.  

Michezo inaweza kutufanya kurejea katika maisha yetu baada ya COVID-19 

Kuelekea siku ya Kimataifa ya Michezo kwa ajili ya Maendeleo na Amani kesho Aprili 6,  ujumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu siku hiyo umeeleza kuwa Mchezo unaweza kusaidia kuchukua jukumu katika kujenga mnepo na katika kupona dhidi ya janga la COVID-19. 

6 Aprili 2020

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)

ASSUMPTA:Ni Jumatatu 06 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI

Sauti -
12'28"

Ulimwengu wa michezo nao umepata pigo kutokana na uwepo wa COVID-19

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani , Umoja wa Mataifa umesema jumuiya ya kimataifa ya michezo inakabiliwa na changamoto kubwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona,

Sauti -
2'25"

Mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote tuunde timu moja dhidi ya COVID-19-WHO na FIFA

Shirikisho la soka ulimwewnguni FIFA limeungana na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO katika kuunga mkono kampeni ya #BeActive yaani #Jishughulishe iliyozinduliwa leo katika Siku ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani ili kuhamasisha watu kuwa na afya wakiwa nyumbani wakati huu ambao dunia inaungana katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19, leo na kila siku.

Jumuiya ya michezo yakabiliwa na changamoto kubwa sababu ya COVID-19 :UN

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani , Umoja wa Mataifa umesema jumuiya ya kimataifa ya michezo inakabiliwa na changamoto kubwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa watu wengi kushindwa kujumuika katika michezo mbalimbali na pia kufanya mazoezi.

Mkakati wa kimatifa wazinduliwa kuhakikisha usalama dhidi ya ugaidi

Wawakilishi kutoka vyama vya michezo vya kimataifa na sekta binafsi wameungana na mabalozi kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Jumatatu ili kuzindua mkakati wa kimataifa  wenye lengo la kulinda hafla kuu za michezo dhidi ya vitisho vinavyohusiana na ugaidi

Kandanda yawaleta pamoja vijana mahasimu Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini

Sauti -
1'46"

Vijana Sudan Kusini pambaneni michezoni lakini sio vitani:UNMISS

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umekamilisha ujenzi wa uwanja wa kandanda nje kidogo ya mji wa Juba lengo kuu likiwa kuwaunganisha wanajamii kupitia michezo.