Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 FEBRUARI 2024

21 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na mabomu ya kutegwa ardhini nchini Ukraine. Makala tukupeleka katika ukanda wa Gaza na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Bintou Keita, ameliambia Baraza la Usalama kwamba ana wasiwasi mkubwa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaofanywa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa M23, ambapo vuguvugu hilo linalenga watendaji wa mashirika ya kiraia, hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.
  2. Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016. 
  3. Makala tunaelekea Gaza ambapo tangu Oktoba 7 mwaka jana kulipozuka machafuko huko Ukanda wa Gaza, wanawake wanaume na watoto wamekuwa wakikimbia kutoka eneo moja Kwenda jingina mpaka sasa wengi wao wapo Rafah karibu kabisa na mpaka wan chi ya Misri lakini umeshajiuliza kwa miezi mitano wanawake wa Gaza wanafanyaje wanapoingia katika kipindi cha hedhi kila mwezi?
  4. Mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama tutaelekea mjini Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania kumsikia kijana anayetumia Kiswahili kama lugha mama.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'55"