Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 FEBRUARI 2024

08 FEBRUARI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimulika hali ya wakimbizi wa ndani na ziara ya  Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi nchini Sudan.Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na neno la wiki tunakuleleta uchambuzi wa methali “Mjinga akierevuka, mwerevu yupo mashakani.”

  1. Huko Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wamesema wanafanya kila liwezekanalo kuwasaidia waathirika wa mafuriko mabaya zaidi nchini humo yaliyosababisha kina cha mto Congo kufurika katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 60. 
  2. Gaza wakati mashambulizi makubwa ya mambomu ya Israel yakiendelea kwa njia ya anga, aridhini na baharini katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza na hususan Khan Younis na viunga vyake  na kuongeza idadi ya vifo, majeruhi na wakimbizi wa ndani shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema jana Februari 7 jeshi la Israel lilitangaza kusitisha kwa muda na kwa kimkakati hii leo operesheni zake za kijeshi katika maeneo ya magharibi mwa Rafah kuanzia saa nne asubuhi hadi saana nane mchana saa za Israel ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia. 
  3. Mkutano wa maandalizi wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea zisizo na bandari (LLDCs), unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York umesema nchi hizo kwa kukosa fursa ya moja kwa moja ya kuwa na bahari      zinakabiliwa na vikwazo vikubwa vya kibiashara, mawasiliano na maendeleo.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Mjinga akierevuka, mwerevu yupo mashakani.”          

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'47"