Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres: Vita, mabadiliko ya tabianchi na AI ni changamoto tunazopaswa kuzishughulikia haraka

Guterres: Vita, mabadiliko ya tabianchi na AI ni changamoto tunazopaswa kuzishughulikia haraka

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis akigusia changamoto mbalimbali zinazpoikabili dunia hivi sasa kuanzia vita inayoendelea Gaza na kwingineko, hali ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya akili mnemba au AI. 

Asante Evarist katika hotuba yake Bwana Guterres alianza kwa kuelezea wasiwasi kuhusu changamoto ya tabianchi na ongezeko la joto duniani akisema nchi zimekumbwa na tabia ya kutochukua hatua na ubinafsi katia masuala ya maendeleo na matumizi ya mafuta kisikuku yameifanya dunia kushindwa kushikamana kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuchochea ongezeko la joto duniani “ Nchi zinaendelea kuzalisha hewa chafuzi, sayari yetu inazidi kuchemka kuelekea nyuzi joto 3celisius, ukame, vimbunga, moto wa nyika na mafuriko winaathiri nchi na jamii.”

Hotuba hiyo pia imegusa kwa kirefu hofu ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa na majanga ya kibinadamu hususan katika mizozo inayoendelea kama vile Gaza na Ukraine akisema kuanzia uvamizi wa Urusi Ukraine hadi Sudan na hivi karibuni kabisa Gaza, pande husika katika mizozo hiyo zinapuuza sheria za kimataifa, zinakiuka mikataba ya Geneva na hata kukiuka katiba ya Umoja wa Mataifa.

“Dunia imesismama ikiangangalia raia hususani wanawake na watoto wakiuawa, kulemazwa, kushambuliwa kwa mabonmu, kufurushwa makwao na kunyimwa haki ya misaada ya kibinadamu.”

Kwa Gaza mathalani amerejea wito wa usitishwaji mapigano mara moja na kuwa na mchakato ambao utaelekea kuleta amani ya kudmu kwa Israel na Palestina  kwa misingi ya kuwa na mataifa mawili akisistiza kwamba “Hii ndio njia pekee ya kukata shina la madhila na kuzuia mzozo huo kusambaa hali ambayo itawasha moto katika ukanda mzima.”

Na kuhusu suala la Akili mnemba Katibu Mkuu amezungumzia hatari yake na uwezekano wa kuongeza pengo la usawa na tabia isiyofaa ya makampuni makubwa ya teknolojia "Teknolojia hii ina uwezo mkubwa wa maendeleo endelevu lakini kama Shirika la Fedha Duniani lilivyotuonya hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa wa kuzidisha ukosefu wa usawa duniani. Na baadhi ya makampuni yenye nguvu ya teknolojia tayari yanafuata faida kwa kutozingatia haki za binadamu, faragha kibinafsi na athari za kijamii,"

Amehitimisha hotuba yake kwa kwa kusisitiza hali muhimu na inayowezekana ya kujenga upya imani kwa ajili ya dunia iliyo salama na imara zaidi.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'37"
Photo Credit
© World Economic Forum